Exodus 20:18-21

18 aWatu walipoona ngurumo na radi, na kusikia mlio wa tarumbeta, na kuuona mlima katika moshi, walitetemeka kwa woga. Wakasimama mbali 19 bna wakamwambia Musa, “Sema nasi wewe mwenyewe, nasi tutakusikiliza. Lakini usimwache Mungu aseme nasi, la sivyo tutakufa.”

20 cMusa akawaambia watu, “Msiogope! Mungu amekuja kuwajaribu, ili kwamba hofu ya Mungu iwakalie, msitende dhambi.”

21 dWatu wakabaki mbali, wakati Musa alipolisogelea lile giza nene mahali pale Mungu alipokuwa.

Sanamu Na Madhabahu

Copyright information for SwhKC